25 July 2015

KWA NINI MAPENZI NI ASALI, VILEVILE NI SHUBIRI?

Kwa nini mapenzi ni tata? Unaweza kujiuliza swali hilo. Ni kwa faida ya kila mmoja kwa sababu yanamhusu kila mmoja wetu. Ni matamu lakini ndani yake hutokea kuwa na ukakasi kama siyo maumivu.Jiulize tena, kwa nini mapenzi yanasumbua? Mapenzi ni maumivu ya kichwa na moyo. Watu wengi waliomo ndani yake wanaweza kukupa ushuhuda wa mateso wanayoyapata kwenye uhusiano wao. Je, baada ya kuteseka huwa wanajiapiza kutorudi tena?

La hasha! Wanajaribu mara nyingi, hawakomi. Unaweza kujiuliza ni kwa nini lakini ukweli ni kwamba pamoja na maumivu ambayo mtu anaweza kuyapata kwenye mapenzi, bado yanabeba hisia kubwa kabisa katika maisha ya kila binadamu.

Maisha bila mapenzi hayajakamilika. Kutokana na hilo, uwanja upo wazi kwako kujiuliza ni kwa nini kitu kitamu namna hiyo kikafanywa kuwa tata, jumlisha na maumivu ya hapa na pale. Uvumilivu ukizingatiwa, huyeyusha utata unaojitokeza hapa na pale.

Muhimu zaidi ni kwamba mapenzi hayatoshelezi kwa uwajibikaji wa nusunusu. Yanahitaji nidhamu na utekelezaji wa moja kwa moja kutoka moyoni. Yanayomhusu mwenzi wako ni vema uyabebe kama yako, hivyo ndivyo uhusiano unavyotaka.

Mapenzi yanahitaji akili, utashi na fikra zako bila kusahau nguvu zote katika kuzalisha matunda ya kila siku kwenye uhusiano ulionao. Utata unaoonekana ni ule unaotokana na wenzi kutotimiza matarajio ya kila mmoja.

Imetokea kuamini kuwa maneno ni mhimili wa kudumu kwa uhusiano na ngono husuluhisha migogoro ya muda mfupi. Wapenzi wanaponuniana, endapo watakutana faragha, hasira zote hupotea. Hata hivyo, kwa bahati mbaya, ni zaidi ya kutosheka kimwili na utamu wa maneno mazuri.Kwa mfano, ndoa nyingi zinakumbwa na matatizo ya watu kushindwa kuwa wakweli. Mwanaume au mwanamke anaweza kusema ni kiasi gani mwenzi wake anamuumiza. Lakini mwisho wa mazungumzo hawezi kukiri kasoro zake ambazo pengine ndiyo chanzo cha kila kitu.

Utata zaidi katika mapenzi ni kuwa inapotokea watu wanajuana kwa undani mno, hasa baada ya kuishi muda mrefu, ni hapo ndipo maneno hayawezi kufaa kitu, wala mchezo wa faragha hautaleta maelewano kwa maana hakuna kitu kigeni. Lingine la utata katika mapenzi ni kwamba huwezi kuficha tabia yako muda wote

6 January 2015

AIBU...!!! MSANII WA BONGO FLEVA MATONYA AFANYIWA USODOMA

Picha hizi zimezagaa kwenye Mitandao tofautitofauti ya kijamii ambazo zimeleta utata na kudai kuwa msani Maararu wa kizazi kipya Matonya baada ya kulewa vijana wa kihuni walimvua nguo na kumfanya kitendo kibaya.... Mtandao huu unajaribu kumtafuta msanii huyu ili kutoa ufafanuzi wa picha hizi ila kwa bahati mbaya hatukufanikiwa kumpata

vijana wa kihuni wakifanya kazi yao

VIONGOZI WA SIASA WAMTAKA RAIS KIKWETE AFANYE MAAMUZI JUU YA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI

Viongozi wa vyama vya siasa nchini wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kutekeleza ahadi yake aliyoahidi wakati wa mkutano na wazee wa Dar es Salaam ya kufanya maamuzi ya kumwajibisha waziri wa nishati na madini ambaye alimweka kiporo na kudai kuwa atatoa maamuzi ndani ya siku mbili lakini hadi leo amekaa kimya.

Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Prof Iibrahim Lipumba amesema suala la viongozi wakiwemo mawaziri kuwajibika halikuanza leo hasa anaposhindwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kuisababishia serikali hasara au kushusha heshima ya taifa hivyo ni vyema uwajibikaji ukawa ni kwa kila mtumishi wa umma bila kubagua ili kuleta tija kwa taifa.

Kwa upande wake mjumbe wa halmashauri kuu taifa ya chama cha mapinduzi CCM Bw Najim Msenga amesema niimani ya chama chake kuwa rais atafanya maamuzi sahihi kwa maslahi ya taifa kama alivyoahidi na kwamba suala hilo haliwezi kuathiri uhai wa CCM kwani bado iko imara baada ya baadhi ya watuhumiwa kuchukuliwa hatua.

Akizungumzia suala hilo katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Dk Willbroad Silaa amesema hata hao waliojiuzulu na kuenguliwa uteuzi wao maadam uchunguzi ulifanywa na vyombo sahihi hadi kufikia hatua ya kupelekwa bungeni na kujadiliwa na wao kutoa maazimio watuhumiwa wote hadi sasa walipaswa wawe wamefikishwa mahakamani.

Katika mkutano wake na wazee wa Dar es Salaam uliofanyika ukumbi wa Diamond Jublee desemba 22 mwaka jana Rais Kikwete alitengua uteuzi wa aliyekuwa waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh Anna Tibaijuka na kutangaza kumweka kiporo waziri wa nishati na madini Prof Muhongo.

NAY WA MITEGO: NIKKI MBISHI ALICHELEWA KUACHA MUZIKI

Nay wa Mitego amempongeza Nikki Mbishi kwa uamuzi wake wake kuachana na muziki.
Hata hivyo Nay amesema Nikki amechelewa mno kufanya hivyo.

“Mtu unaweza kuangalia hiki hakinifai bora niende upande mwingine labda unaweza ukagharamia kitu ukakuta sio sehemu ambayo umepangiwa, ukaenda ukajaribu kitu kingine ukakuta maisha ni rahisi na yanaenda, Nay amekiambia kipindi cha Power Jams cha East Africa Radio. “Sijui kwanini alikuwa anachelewa, nimefurahi kuona maamuzi mazuri kijana mwenzangu amejitambua na kuamua kuangalia vitu vingine. Kama bado hajapata cha kufanya aje mimi nimshauri afanye nini.

KWA NINI MAPENZI NI ASALI, VILEVILE NI SHUBIRI?

Kwa nini mapenzi ni tata? Unaweza kujiuliza swali hilo. Ni kwa faida ya kila mmoja kwa sababu yanamhusu kila mmoja wetu. Ni matamu lakini ndani yake hutokea kuwa na ukakasi kama siyo maumivu.Jiulize tena, kwa nini mapenzi yanasumbua? Mapenzi ni maumivu ya kichwa na moyo. Watu wengi waliomo ndani yake wanaweza kukupa ushuhuda wa mateso wanayoyapata kwenye uhusiano wao. Je, baada ya kuteseka huwa wanajiapiza kutorudi tena?

La hasha! Wanajaribu mara nyingi, hawakomi. Unaweza kujiuliza ni kwa nini lakini ukweli ni kwamba pamoja na maumivu ambayo mtu anaweza kuyapata kwenye mapenzi, bado yanabeba hisia kubwa kabisa katika maisha ya kila binadamu.

Maisha bila mapenzi hayajakamilika. Kutokana na hilo, uwanja upo wazi kwako kujiuliza ni kwa nini kitu kitamu namna hiyo kikafanywa kuwa tata, jumlisha na maumivu ya hapa na pale. Uvumilivu ukizingatiwa, huyeyusha utata unaojitokeza hapa na pale.

Muhimu zaidi ni kwamba mapenzi hayatoshelezi kwa uwajibikaji wa nusunusu. Yanahitaji nidhamu na utekelezaji wa moja kwa moja kutoka moyoni. Yanayomhusu mwenzi wako ni vema uyabebe kama yako, hivyo ndivyo uhusiano unavyotaka.

Mapenzi yanahitaji akili, utashi na fikra zako bila kusahau nguvu zote katika kuzalisha matunda ya kila siku kwenye uhusiano ulionao. Utata unaoonekana ni ule unaotokana na wenzi kutotimiza matarajio ya kila mmoja.

Imetokea kuamini kuwa maneno ni mhimili wa kudumu kwa uhusiano na ngono husuluhisha migogoro ya muda mfupi. Wapenzi wanaponuniana, endapo watakutana faragha, hasira zote hupotea. Hata hivyo, kwa bahati mbaya, ni zaidi ya kutosheka kimwili na utamu wa maneno mazuri.Kwa mfano, ndoa nyingi zinakumbwa na matatizo ya watu kushindwa kuwa wakweli. Mwanaume au mwanamke anaweza kusema ni kiasi gani mwenzi wake anamuumiza. Lakini mwisho wa mazungumzo hawezi kukiri kasoro zake ambazo pengine ndiyo chanzo cha kila kitu.

Utata zaidi katika mapenzi ni kuwa inapotokea watu wanajuana kwa undani mno, hasa baada ya kuishi muda mrefu, ni hapo ndipo maneno hayawezi kufaa kitu, wala mchezo wa faragha hautaleta maelewano kwa maana hakuna kitu kigeni. Lingine la utata katika mapenzi ni kwamba huwezi kuficha tabia yako muda wote

HURUMA JAMANI! MTOTO HUYU MDOGO ANAISHI NA UTUMBO WA PLASTIKI

Mtoto mwenye matatizo ya tumbo, Suleiman Abdallah.

Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Veronica Laurent, mkazi wa Magomeni Mwembechai, jijini Dar, amejikuta kwenye wakati mgumu kwa kutelekezwa na mzazi mwenzie baada ya kujifungua mtoto akiwa na matatizo ya utumbo.Akizungumza na mwandishi wetu Veronica alisema mwanaye Suleiman Abdallah (4), alipozaliwa tu, choo chake hakikutoka kwa njia ya kawaida bali kilitokea mdomoni huku manesi wakisema ana utumbo mkubwa na moja kwa moja alichukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na hali yake kuwa mbaya.
Sehemu ya tumbo la mtoto Suleiman Abdallah iliyofanyiwa upasuaji.

AWEKEWA UTUMBO WA PLASTIKI
“Tulipofika pale Muhimbili mwanangu aliwekewa mashine ya kupumulia na baada ya kumchukua vipimo waligundua kuwa utumbo mkubwa wa choo umejifunga wakasema itabidi alazwe kwa ajili ya upasuaji ambapo alipasuliwa na kuwekewa utumbo wa plastiki ambao anaishi nao mpaka leo.
“Sasa tukaandikiwa tuwe tunahudhuria kliniki kila mwezi kutokana na tarehe husika lakini mwezi uliopita mtoto alianza kulalamika kuwa anasikia maumivu makali ya tumbo na hapati choo kabisa na hata akipata ni kidogo sana.
Kovu la upasuaji tumboni mwa mtoto Suleiman Abdallah.

“Tulienda hospitali tukapewa dawa za kutuliza maumivu tu na madaktari walishasema kama mtoto ana maumivu ya tumbo tumpeleke kwenye hospitali ya karibu, Muhimbili ni kwa ajili ya kliniki yake tu,” alisema mama huyo huku akitokwa machozi.

BABA AMTELEKEZA
Mama huyo anaelezea kuwa yeye ndiye mlezi wa mtoto huyo baada ya kutelekezwa na mzazi mwenzie ambaye alidai hajali kumhudumia.
“Baba wa mtoto alipoona mwanaye ana matatizo haya alisema hanihitaji mimi na mtoto niende nikatafute mtu wa kunisaidia na yeye atatafuta mwanamke mwingine wa kuzaa naye pia nilishawahi kupigwa na shangazi yake kwa madai kuwa namsumbua mwanaye.
Veronica Laurent ambaye ni mama mzazi wa mtoto Suleiman Abdallah.

APASULIWA MARA NNE
“Nimekuwa nikihangaika mwenyewe kwa miaka yote tangu alipozaliwa na tayari ameshapasuliwa mara nne tangu azaliwe lakini bado tatizo linaendelea kumtesa mtoto.
“Kwa sasa naomba serikali inisaidie kama inawezekana naomba mwanangu achunguzwe tena kwa sababu sasa hivi analalamika sana na hata tumbo lake linajaa,” alisema na kuongeza kuwa ili apasuliwe tena zinahitajika fedha shilingi 1,000,000 ambazo hana hata senti tano.

Ili kuweza kufanikisha upasuaji huo wewe uliyesoma habari hii unaombwa kumsaidia mama huyu kwa kiasi chochote ulichonacho na Mungu atakupa baraka zake.
Aliyeguswa na kuhuzunishwa na mateso ya mtoto Suleiman anaweza kuchangia kupitia namba ya simu 0712 004 677 na 0767 026 551

MWALIMU AONGOZA KWA KUPIGWA NA MUME WAKE, MBAYA SANA

Hali aliyokuwa nayo mwalimu Gaudencia Gitano baada ya kipigo cha mwaka 2012.Mwalimu Gaudencia Gitano (40) anayefundisha Shule ya Msingi Kivelu jijini Dar es Salaam, amedai huenda yeye ndiye anayeongoza kwa kupigwa kuliko wanawake wengine wote jijini, baada ya kudai anazo RB tano za vipigo tofauti kutoka kwa mumewe kwa nyakati mbalimbali tangu aolewe Oktoba 25, 2002, katika ndoa ya kiserikali iliyofungwa Ilala Boma.

Mwalimu Gaudencia Gitano (40) anayedai kupigwa mara nyingi na mume wake.
Akizungumza akiwa kitandani katika Hospitali ya Dar Group iliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, Gaudensia (pichani), alidai kupigwa mara kwa mara kiasi kwamba katika vituo vya polisi na hospitali, amekuwa ni mwenyeji.
“Mimi ni mke wa pili kati ya watatu na tulifunga ndoa ya kiserikali na mume wangu Colman Marwa Oktoba 25, 2002 huko Ilala Boma. Tulikuwa tukipendana na Mungu ametujaalia tumepata watoto wawili, tulikuwa tukiishi pamoja katika nyumba yetu huko Kitunda na baadaye tukahamia katika nyumba yetu nyingine huko Msongola